Alhamisi , 20th Jul , 2023

Inaelezwa kuwa nchi nyingi za Afrika zinakabiliwa na hali ngumu ya uchumi na ndio maana kwa baadhi ya nchi kumekuwa na migogoro hii ni kutokana na mfumuko wa bei hususani kwenye vyakula

Nafaka mbalimbali

Hayo yamebainishwa na Walter Nguma Mtaalam wa Uchumi wakati akizungumza kwenye kipindi cha Supa Breakfast kinachoruka kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kupitia East Africa Radio na kusema kuwa mfumuko wa Bei hasa kwenye Chakula ndio changamoto kubwa

"Ugumua wa maisha ni suala ambalo linaonekana katika nchi nyingi za Afrika na hali inaonekana sio nyepesi na ndio maana hata Kenya unaona yanayoendelea ni kwa sababu ya hali ngumu ya maisha lakini pia ukienda Afrika ya kati,Congo bado kuna changamoto na sababu kuu ni mfumuko wa bei hasa kwenye vyakula," Anasema Walter Nguma.

Akizungumzia kwa Tanzania hasa kwa mtu mmoja mmoja Walter anasema  bado kuna kundi kubwa la watu ambao hawana ajira,kuna kundi kubwa pia ambao wanafanya biashara na haziendi vizuri na pia wapo ambao wanategemea ndugu kuweza kuishi.

Mwisho anasema katika nchi yoyote maisha hayawezi kuwa sawa kwa kila mtu hata ukienda kwenye mataifa makubwa ambayo yameendelea bado kuna watu amba o wana lalamika maisha magumu hivyo mtu akuilalamika kuhusu Ugumu wa maisha lazima umuelewe.