Amesema lengo la serikali ni kuweka mazingira rafiki ya watu kufanya biashara ambapo amesema ili serikali iendelee kuweka mazingira rafiki amewataka wawezekaji kulipa kodi kwa wakati ili wananchi waendelee kupata maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara na miundombinu mbalimbali
Profesa Kitila amesema moja ya lengo la serikali la kupunguza Makampuni na kuuganisha baadhi ya kampuni na taasisi ni ili Kupunguza kiwango cha usimamizi ambapo kwasasa taasisi nyingi zilikuwa zinafanya kazi zinazonana