Jumatano , 20th Jul , 2022

Serikali kupitia kituo chenye dhamana ya uwekezaji nchini TIC imepokea ujumbe wa wawekezaji kutoka jumuiya ya nchi za kiarabu kwa ajili ya kufanya fursa za uwekezaji kwenye sekta mbalimbali ikiwemo mifugo.

Ujumbe huo uliopokelewa na Naibu waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Exaud Kigahe umelenga kutazama maeneo ya uwekezaji katika sekta za kilimo Ili kuhakikisha usalama wa chakula kwa nchi za kiarabu ambazo kwa asili mazingira yake ni jangwa.

Ujumbe huu unatajwa kama ishara njema kufuatia ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini Oman mapema mwezi Juni 2022.

Katika maeneo ambayo wamevutiwa nayo na kutembelea ni Ranchi ya Taifa, mamlaka ya maeneo maalumu ya uwekezaji kwa mauzo ya nje EPZA, SUMA JKT, Bodi ya nafaka na mauzo mchanganyiko pamoja na Bodi ya nyama.