
Kariakoo soko la kimkakati likitajwa kama kitovu cha biashara ambalo mataifa mbalimbali ya jirani hununua bidhaa hapa ambapo Rai imetolewa na meneja wa TRA mkoa wa kikodi wa kariakoo kwamba wamejipanga kuhakikisha wateja wanakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu kodi na taarifa sahihi.
Hata hivyo amesema kwa sasa mamlaka inajipanga zaidi kuitumia teknolojia kwa usajili wa wamachinga ambapo hadi sasa zaidi ya wafanyabiashara wadogo maarufu kama wamachinga 5373 wamesajiliwa
Licha ya soko la kariakoo kuwa na eneo dogo la kijiografia lenye square mita za mraba 3.47 linatajwa kuwa na wafanyabiashara takribani elfu thelathini ambapo kwa kipindi hiki mamlaka imejipanga kukusanya takribani shilingi bilioni 19.5.