Jumatatu , 21st Nov , 2022

Serikali imeyataka makampuni yanayotoa Huduma za mawasiliano kutoongeza gharama ama kufanya mabadiliko yeyote mpaka pale tathimini ya ambayo tayari imeanza itakapokamilika.

Waziri wa Habari na Mawasiliano-Nape Nnauye

Tayari imeanza Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa habari na mawasiliano Nape Nnauye kabla ya kikao cha wadau wa mawasiliano kilichokuwa na lengo la kukusanya maoni na kujadili mamambo ambayo wadau wanatamani kuyaona katuika sheia mpya ambapo amesema tathimini ya mwisho ilifanyika mwaka 2018 na nyingine inafanyika mwka huu ikitegemewa kukamilika kati ya mwezi December na January.

Nape amesema Kwa sasa Hali inaonesha kutokuwepo Kwa mahusiano mazuri kati ya watoa huduma na watumiaji wa Huduma za mawasiliano hivyo serikali imeamua kufanya tathimini ya kina ambayo itakuja na majibu ya gharama gani zitumike kwenye bando usafirishaji wa data,ulipaji wa Kodi uwekezaji na masuala mengi ya kiuendeshaji

“Naomba ieleweke hivi kwa sasa hakuna mabadiliko yeyote kwenye huduma za mawasiliano mpka pale ambapo tathimini itakamilika na hii yote imefikiwa kufuatia kulalamika sana kwa watumiaji wa huduma”amesema waziri Nape.

Hata hivyo ametoa wito kwa wadau kujitokeza kuomba nafasi kwenye baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano baraza ambalo kwa sasa liko na wajumbe wachache kiasi ambacho liashindwa kutekeleza majukumu yake.