EATV yakamilisha hivi wiki ya huduma kwa wateja

Ijumaa , 9th Oct , 2020

Kituo cha redio cha East Africa Radio, kupitia kipindi chake cha Supa Breakfast kwa kushirikiana na Royal Oven Bakery leo wamekamilisha kampeni ya kutoa zawadi kwa watoa huduma bora ambapo imekabidhi makapu mawili kwa Mwalimu pamoja na Daktari kutoka hospitali-

Muandaaji wa kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio, Mackriner Siyovelwa akimkabidhi zawadi kutoka Royal Oven Bakery, Dkt. Ahmed Mussa Kashagama (Kash) Daktari bingwa wa Wanawake kutoka hospitali ya Rabinsia (kulia), pamoja na Mwl. Vicent Mganga kutoka shule ya msingi na awali ya Divine iliyopo Salasala jijini Dar es Salaam, kwa niaba East Africa TV na East Africa Radio katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.

ya Rabininsia ya Jijini Dar es Salaam.

Kampeni hiyo ya kuwazawadia watoa huduma bora katika Wiki ya Huduma kwa Wateja iliendeshwa kupitia wasikilizaji wa East Africa Radio ambao walipiga simu na kuelezea namna ambavyo dawati la kutoa huduma kwa mteja katika taasisi husika lilivyosaidia kutatua tatizo lao.

Akizungumza baada ya kupatiwa kapu hilo Mwalimu Vicent Mganga kutoka shule ya msingi na awali ya Divine iliyopo eneo la Salasala nje kidogo mwa Jijini Dar es Salaam, amesema kuwa ualimu ni wito na kuwataka walimu wenzake kufanya kazi kwa upendo kwa wanafunzi.

Kwa upande wake mshindi wa pili kwa hii leo ambaye ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake kutoka hospitali ya Rabininsia, Dkt. Ahmed Mussa Kashagama (Kash) amesema kuwa kazi ya hudumu ya afya haiishii tu kumpa mgonjwa dawa bali kuhakikisha anakuwa na afya njema.