Jumanne , 2nd Aug , 2022

Bei ya mafuta kuanzia kesho Agosti 3, 2022, kwa mkoa wa Dar es Salaam, Petroli itauzwa shilingi 3,410, Dizeli 3,322 na mafuta ya taa yatauzwa kwa shilingi 3,765, Tanga Petroli itauzwa 3,435 na Dizeli itauzwa 3,349.

Kituo cha mafuta

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumanne Agosti 2, 2022 na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) na kusema petroli mkoani Mtwara itauzwa 3,393kwa lita na dizeli itauzwa 3,351 kwa lita.

Aidha bei ya petroli kwa Arusha ni 3,492 kwa lita na dizeli ni shilingi 3,406