
Washehereshaji wa Onesho la Dance100% Tony Albert au T - Bway na Menina Atick wakionesha uwezo wao wa kusakata dansi wakati wanaingia katika usaili wa Tatu na wa mwisho uliofanyika katika viwanja vya mpira wa kikapu TCC - Chang'ombe - DSM.

Tony Albert au T-Bway na Menina Atick wakisakata dansi kabla ya mashindano Dance100% katika usaili wa mwisho kuanza katika viwanja vya TCC-Chang'ombe yaliyofanyika tarehe 3/8/2014 jijini Dar es salaam. Mashindano yanadhaminiwa na Vodacom-Tanzania

Mmoja wa majaji wa Shindano la Dance100% Hassan Nyamwela almaarufu kama Super Nyamwela akiingia kwa madoido ya kudansi katika viwanja vya TCC-Chang'ombe katika mashindano hayo yaliyofanyika tarehe 3/8/2014.

Jaji Queen Darleen akiingia kwa kucheza kwa manjonjo katika mashindano ya Dance100%

Baadhi ya mashabiki na wafuatiliaji wa mashindano ya Dance100% wakiangalia kwa makini kinachoendelea katika mashindano hayo katika viwanja vya TCC - Chang'ombe, Mashindano ya #2014Dance100 yanadhaminiwa na Vodacom na kinywaji rasmi ni Grand Malt.

Kundi la Best Boys Crew likionyesha mbwembwe za kudansi katika mashindano ya usaili wa tatu na wa mwisho ya Dance100% yaliyofanyika katika viwanja vya mpira wa kikapu TCC - Chang'ombe tarehe 3/8/2014

Kundi la Best Boys Crew likionesha manjonjo yao ya kudansi katika mashindano ya usaili wa Tatu na wa mwisho ya Dance100% mnamo tarehe 3/8/2014 katika viwanja vya TCC - Chang'ombe jijini Dar es salaam.

Kundi la Dar Crew likionesha mbwembwe za kudansi katika mashindano ya usaili wa tatu na wa mwisho ya Dance100% viwanja vya TCC - Chang'ombe. mashindano yanadhaminiwa na Vodacom Tanzania huku kinywaji Rasmi kikiwa ni Grand Malt.

Jaji Lotus Kyamba akitoa alama zake kwa kundi husika katika mashindano ya Dance100%, kinywaji rasmi cha mashindano hayo ni Grand Malt huku yakiwa yanadhaminiwa na Vodacom Tanzania

Kundi la The W-T likitoa ubunifu wake wa kuDansi katika mashindano ya usaili wa 3 na wa mwisho katika viwanja vya TCC - Chang'ombe yaliyofanyika tarehe 3/8/2014

Washehereshaji wa mashindano ya kudansi ya Dance100% Tony Albert ama T-Bway na Menina Atick wakiongea na kundi la The W-T baada ya kumaliza kuonesha ubunifu wao wa kudansi.

Kundi la G.O.P likitoa ubunifu wake wa kuDansi katika mashindano ya usaili wa 3 na wa mwisho katika viwanja vya TCC - Chang'ombe yaliyofanyika tarehe 3/8/2014.

Kundi la G.O.P likionesha manjonjo yao ya kudansi katika mashindano ya usaili wa 3 na wa mwisho ya Dance100% mnamo tarehe 3/8/2014 katika viwanja vya TCC - Chang'ombe jijini Dar es salaam.

Jaji Hassan Nyamwela kwa jina maarufu Super Nyamwela akitoa alama zake kwa kundi husika katika mashindano ya Dance100% , kinywaji rasmi cha mashindano hayo ni Grand Malt huku yakiwa yanadhaminiwa na Vodacom Tanzania

Baadhi ya mashabiki na wafuatiliaji wa mashindano ya Dance100% wakiangalia kwa makini kinachoendelea katika mashindano hayo katika viwanja vya TCC - Chang'ombe, Mashindano ya #2014Dance100 yanadhaminiwa na Vodacom na kinywaji rasmi ni Grand Malt.

WAZAWA CREW

Kundi la Mwanzo Mwisho ni moja ya makundi yaliyojitokeza katika usaili wa 3 na wa mwisho katika mashindano ya Dance100% yaliyofanyika katika viwanja vya TCC - Chang'ombe tarehe 3/8/2014 likionyesha jitihada zake za kudansi.

STREET DANCER

Washehereshaji mashindano ya Dance100% wakiwa na makundi yaliyofanikiwa kuvuka mchujo wa usaili wa 3 wa mwisho yaliyofanyika katika viwanja vya TCC, makundi hayo Sita ni Dar Crew, Best Boys Crew, The W-T, G.O.P, Best Love na Wazawa Crew.