Yanga yaweka wazi mpango wake dhidi ya Kengold FC

Ijumaa , 26th Feb , 2021

Mabingwa wa zamani wa kombe la Shirikisho nchini, Klabu ya Yanga kesho tarehe 27 Februari 2021 mishale ya saa 10:00 jioni inatazamiwa kushuka dimbani kukipiga dhidi ya klabu ya Kengold ya Chunya, jijini Mbeya kwenye mchezo wa mzunguko wa nne wa michuano hiyo.

Baadhi ya wachezaji wa Yanga, wakishangilia moja ya bao kwenye VPL msimu huu.

Kuelekea kwenye mchezo huo, Kocha wa klabu ya Yanga, Cedric Kaze amesema, “Kwenye mchezo wa mtoano, kila mtu anauwezo wa kujitolea kwenye dakika tisini bila kujali anatakea kwenye ligi daraja la ngapi.”

“Sasa ni mechi ambayo tutaicheza kwa tahadhari kubwa kwani tumejiandaa vizuri kwasababu tunajua kama Kengold ni timu ambayo ipi kwenye muelekeo mzuri.”

Kengold ipo nafasi ya tatau baada ya kucheza michezo kumi, sare mchezo mmona na kupokea vipigo vinne na kuwafanya kufikisha alama 16 wakati, Yanga ni kinara wa VPL akiwa na alama 49 licha ya kuwa michezo mitatu mbele ya mabingwa watetezi, Wekundu wa Msimbazi Simba.

Kwa upande wa wachezaji, kinara wa mabao wa klabu ya Yanga, kiungo, Deus Kaseke amesema “Kila mchezaji ana nia na hamu ya kucheza mechi hiyo na nina amini tutashinda kwa uwezo wa Mwenyeenzi Mungu.”

Kuhusu hali ya wachezaji, inaelezwa kuwa mshabuliaji Said Ntibazonkiza huenda akaendelea kukosekana kikosini kutokana na majeraha ilhali mshambuliaji Yacouba Sogne amerejea na kufanya mazoezi ya pamoja na timu.

Michezo mingine ya Shirikisho itakayopigwa hapo kesho, ni Polisi TZ dhidi ya Kwamndolwa saa 8:00 mchana pamoja na ule wa Azam watakapowakaribisha Mbuni kwenye dimba la Chamazi jijini Dar es Salaam saa 1:00 usiku.