Siyo bahati Azam FC kuifunga Yanga 4-0- Cheche

Sunday , 8th Jan , 2017

Kocha wa Azam FC Iddy Cheche amesema matokeo ya jana dhidi ya Yanga hayamfanyi kuwa katika njia ya kupata nafasi ya Ukocha mkuu wa Azam FC.

Kocha wa Azam FC Iddy Cheche.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Iddy amesema wapo makocha ambao wamefanya vizuri zaidi katika timu zao na wakatimuliwa.

“Wapo makocha waliofanya vizuri zaidi katika timu zao na wakaambiwa kazi basi, mimi nafanya kazi na uongozi utaangalia,” alisema Cheche.

Akiuzungumzia kwa upande wa matokeo Cheche amesema, wanafuraha kupata ushindi kwani katika mechi za awali timu ilikuwa inatengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini tatizo lilikuwa umaliziaji hivyo walilifanyia kazi hivyo matokeo wameyaona.

“Siyo bahati kushinda nne 4-0 na tungeweza kushinda hata zaidi ya nne kwani tangia tunaanza mashindano na hata katika mchezo huu dhidi ya Yanga wachezaji wangu walikuwa wakipata nafasi nyingi za kufunga na tatizo lilikuwa ni umaliziaji hivyo kabla ya mechi ilibidi nitumie muda kurekebisha na matokeo tumeyaona,” alisema Cheche.

Cheche amesema, kwa sasa najipanga kwa ajili ya nusu fainali na yupo tayari kupambana na timu yoyote kwani anajua yupo vitani na anaamini Ubingwa wa mwaka huu utaenda Azam FC.

Recent Posts

Waziri wa Kilimo, Mifubo na Uvuvii, Dkt. Charles Tizeba

Current Affairs
Tuna chakula cha kusaza - Waziri Tizeba

Mzee majuto katika bustani yake

Entertainment
Mambo matatu kubadili maisha ya mzee Majuto 2017

Moja ya ndege ya mpya za ATCL

Current Affairs
Nauli ya Dar - Dodoma kwa Bombadier, yatajwa

Jumaa Aweso, Mbunge wa Pangani

Current Affairs
Mbunge wa Pangani alia na upungufu walimu

Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi

Sport
Mwambusi apania kuikamata Simba kileleni