Ijumaa , 7th Jan , 2022

Newcastle United imefanikiwa kupata sahihi ya beki wa kulia, Kieran Trippier kutoka Atletico Madrid paundi million 12 sawa na 37,501,300,080 za kitanznaia kwa kandarasi ya miaka mitatu.

Kieran Trippier akisaini kandarasi ya miaka mitatu.

Trippier anakuwa usajili wa kwanza klabuni hapo tangu timu hiyo inunuliwe na matajiri wa Saudi Arabia mwezi Oktoba mwaka jana.

Baada ya kujiunga na Newcastle, beki huyo wa zamani wa Tottenham Hotspurs "Nimefurahi kujiunga na klabu hii nzuri," alisema Trippier, ambaye amekubali mkataba hadi mwisho wa msimu wa 2023-24.

Eddie Howe, aliyeteuliwa kuwa meneja wa Newcastle mwezi Novemba, pia alimsajili Trippier mwaka 2012 wakati akiwa kocha wa Burnley.

Trippier alisema: "Nilifurahia sana wakati wangu huko Madrid, lakini nilipofahamu nia ya Newcastle United, na baada ya kufanya kazi na Eddie Howe hapo awali, nilijua hapa ndipo natakiwa kuwa."

Beki huyo wa kulia wa Uingereza, ambaye alishinda taji la Uhispania na Atletico msimu uliopita, alikuwa amesalia na miezi 18 kwenye mkataba wake.

Newcastle wanashika nafasi ya pili kutoka mwisho kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza, wakiwa wameshinda mchezo mmoja wa ligi msimu huu.