Jumamosi , 8th Jan , 2022

Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba hatorejea dimbani hivi karibuni kufuatia jeraha la kifundo cha mguu kinachomsumbua hadi hivi sasa.

Kocha wa muda wa Manchester United, Ralf Rangnick ameweka wazi kuwa nyota huyo atakuwa nje ya uwanja angalau kwa mwezi mmoja zaidi kufuatia jeraha hilo.

Pogba ambaye anatarajiwa kupewa mkataba wa kuendelea kusalia Manchester United huku ikisemekana atakuwa akilipwa mshahara mkubwa kuliko wachezaji wote katika Ligi Kuu ya Uingereza, aliumia akiwa katika majukumu ya timu yake ya Taifa ya Ufaransa mwezi Novemba mwaka jana.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28, amesalia na miezi sita katika Mkataba wake na yupo huru kufanya mazungumzo na timu yoyote inayomuhitaji.

Ameichezea Manchester United mechi 13 tu katika mashindano yote kabla ya kupata majeraha hayo yanayosababisha akosekane dimbani kwa muda mrefu