Jumatano , 6th Dec , 2023

Shirikisho la Soka la Afrika Kusini (SAFA) limewafungia maafisa kumi wa kamati ya utendaji ya shirikisho hilo ambao wanatoka Chama cha Soka cha Thulamela katika jimbo la Limpopo.

Hii ni kutokana na kuwepo kwa mvutano wa madaraka kati ya SAFA mjini Vhembe na viongozi wa moja ya washirika wake kwenye Chama cha Soka cha Thulamela .

Sakata la kufungiwa kwa viongozi hao limekuja baada ya THULFA kufanya uchaguzi uliokuwa na ushindani mkubwa ambao ulifuatiwa na mizozo, na hivyo Wakati mkoa ulitaka kuingilia kati, viongozi waliochaguliwa walikaidi, hali iliyosababisha suala hilo kupelekwa katika ngazi ya kitaifa na kuamuliwa kwa upande wa mkoa. Hata hivyo Viongozi waliosimamishwa kazi pia walipeleka suala hilo FIFA lakini wakatupiliwa mbali.

Wajumbe wa kamati ya utendaji waliopigwa marufuku ni; David Khakhu , na Eric Munyai . Mavis Mulibana na Eric Makungo . pamoja na viongozi wa kanda tofauti kutoka LFA; Richard Mutego , na Emmanuel Mulaudzi . Thinawanga Maphagela na Nesane Mutshafa .