Kiduku amsifu Waziri Mwakyembe

Jumatano , 14th Oct , 2020

Bondia Mtanzania Twaha Kiduku amesema hamasa katika ndondi imetokana na waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Dkt Harrison Mwakyembe kuunda kamisheni ya ngumi ambayo imekuwa inatetea masilahi ya mabondia.

Waziri mwenye dhamana ya michezo Dokta Harrison Mwakyembe akizungumza na Waandishi kwenye moja ya mkutano.

Akizungumza na East Africa Radio, Twaha Kiduku amesema kuundwa kwa kamisheni hiyo kumepunguza utapeli kwa mapromota ambao walikuwa wanawachezaji mabondia bila kuwalipa stahiki zao.

''Kuundwa kwa kamisheni kumengoza thamani kwa mabondia kuliko ambavyo ilikuwa awali, mapromota walikua wakiwadhulumu sana hata kama walishakubaliana kwenye mikabata'' Twaha Kiduku Bondia.

Kwa upande mwingine bondia huyo amesema wadau wengi wamekuwa wanabeza ushindi wa pointi kwa kwa mabondia hivyo yeye anaahidi kushinda Oktoba 30 dhidi mthailand Sirimonghkon Iamthuam.