Jumatatu , 11th Dec , 2023

Timu ya Girona imerejea tena kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu soka nchini Hispania La Liga baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya FC Barcelona usiku wa kuamkia leo. Wamefikisha alama 41 na wanaongoza Ligi kwa tofauti ya alama 2 dhidi ya Real Madrid wanaoshika nafasi ya pili.

Wachezaji wa Girona wakishangilia baada ya kufunga bao kwenye ushindi wa mabao 4-2 walioupata jana usiku dhidi ya FC Barcelona.

Mabao ya ushindi ya Girona dhidi ya FC Barcelona yamefungwa na Miguel Gutierrez, Artem Dovbyk, Valery Fernandez na Cristhian Stuani. Na yale ya Barcelona yamefungwa na Ilkay Gundogan na Robert Lewandowski. Kwa matokeo ya mchezo huu FC Barcelona imesalia na alama zake 34 wapo nafasi ya 4 kwenye msimamo ikiwa ni tofauti ya alama 7 dhidi ya Girona wanaoongaza Ligi wakiwa na alama 41.

Girona wameishusha Real Madrid kwenye msimamo baada ya Madrid kutoka sare ya bao 1-1 na Real Betis mchezo uliochezwa jumamosi Disemba 9. Kwenye msimamo wa Ligi hiyo nafasi ya 3 wapo Atletico Madrid wana alama 34 sawa na FC Barcelona lakini Barca wamecheza michezo 16 mchezo mmoja zaidi ya Atletico Madrid.