Jumatatu , 11th Apr , 2022

Harusi ya Brooklyn Beckham mtoto wa mchezaji mstaafu wa Uingereza, David Beckham iliyofanyika wikiendi iliyopita imegharimu kiasi ya $3.5m sawa na Tsh billion 8.1

Brooklyn alifunga ndoa na Nicola Peltz, mtoto wa mfanyabiashara mkubwa Marekani, Nelson Peltz mwenye utajiri wa Tsh trillioni 3.7 kwa mujibu wa jarida la Forbes.

Harusi hiyo ilifungwa katika nyumba ya kifahari ya Nelson Peltz yenye thamani ya zaidi ya Tsh billioni 200 katika mji wa Florida.

 

Brooklyn na Nicola walikuwa marafiki tangu wakiwa watoto na wamepisha miaka minne, Brooklyn akiwa na miaka 23 na Nicola miaka 27