Mama wa Konnektion alianzisha upya kwa wapendanao

Jumatatu , 8th Feb , 2021

Mtangazaji wa kipindi cha Drive Show ya East Africa Radio, Ireen Tillya 'Mama wa Konnektion' ametangaza kampeni mpya ya 'tumeshalipia jambo lako' kuelekea siku ya wapendanao ambapo watawawezesha wapenzi au wanandoa kupata chakula cha usiku kwenye hotel zenye hadhi hapa nchini.

Mtangazaji wa East Africa Radio Ireen Tillya

"Waliopo kwenye mahusiano wanatakiwa wasikilize vipindi wanaweza kuambiwa wa-post picha wakiwa na  wapenzi wao na kutumia hashtag zetu za tumeshalipia jambo lako na nogesha mahaba, wengine watapiga simu kueleza kwanini wanastahili kushinda ofa hiyo na wengine wataweza kuelezea mahusiano ya watu wengine wanaowapenda na wanaona wanastahili kupata ofa

"Vigezo ni kwamba lazima uwe na mpenzi, mke, mume au mchumba, pili uweze kujibu maswali yetu tunapokuuliza na kitakachofanyika ni kudhamini dinner au launch yako na mpenzi wako, kwa hapa Dar wataenda Golden Tulip Masaki, kama upo Moshi, Kilimanjaro ni Kili Wonders Hotel na Mwanza wataenda Lahe Hotel" ameongeza Ireen Tillya 

Zaidi mtazame hapa chini kwenye video.