"Alivyokuja nilipata hofu ya maisha"-Mwamy Mlangwa

Jumatano , 15th Jul , 2020

Mjasiriamali wa Kilimo Mwamy Mlangwa, amesema alipata wasiwasi na hofu ya maisha baada ya kuambiwa anataka kutembelewa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.

Msemaji Mkuu wa Wanawake Maryam Kitosi na Mjasiriamali Mwamy Mlangwa

 

Akizungumza na Msemaji Mkuu wa Wanawake Maryam Kitosi, Mwamy Mlangwa ameeleza kuwa alivyotembelewa alipata hofu ya maisha kwa sababau kutembelewa na Rais sio jambo la kawaida.

"Kuna vitu ukikaa Duniani ukivifikiria unatamani vikutokee ila vikikutokea unapata wasiwasi,  siku alivyonitembelea sikuamini ila najua Mh Rais anapenda vitu vya kilimo na vya kimaendeleo, alivyokuja nilipata hofu ya maisha kwa sababu kutembelewa na Rais sio jambo la kawaida, nashukuru alivyoniona kwenye mitandao ya kijamii, pia aliniambia elimu na uzoefu ninayoitumia nisikae nacho peke yangu" amesema Mwamy Mlangwa

Aidha amesema mwaka huu amejipanga kutia nia kwenye nyanja ya uongozi kuanzia Ubunge wa Jimbo, Ubunge wa viti maalum au Udiwani,  "Mungu akinijaliia nitakuwa miongoni mwa watia nia mwaka huu, nitagombea nikichaguliwa sawa nisipochaguliwa pia sawa, naweza nikipata Udiwani, Ubunge wa Viti Maalum au Ubunge wa Jimbo".