Ijumaa , 24th Sep , 2021

Maua Sama ameachia wimbo wake mpya ambao alidokeza ujio wake siku ya jana ambapo Malkia huyo wa muziki wa Bongo Fleva ameonyesha kuumizwa na tabia za mme wake ambaye anachepuka na Zai.

Picha ya msanii Maua Sama

Kwenye moja ya line za hit hiyo inasema ‘’si halali kibudu we hubagui cheupe chekundu, Zai najua ndio sababu kwenye penzi langu nipate tabu’’, huku akumsisitiza Zai amuache mume wake.

Wimbo huo ni wa pili kutoka kwa Maua ndani ya wiki moja baada ya ''Away'' aliomshirikisha Rapper Young Lunya huku zote zikiwa zimepikwa na producer Mr. Simon