Jumatatu , 26th Sep , 2016

Kundi lililoibuka na taji la Dance100% 2016 Timu Makorokocho limesema limetimiza ahadi yao kwa mashabiki wao kwamba mwaka huu utakuwa mwaka wao wa mwisho kushiriki shindano la Dance100%.

Kundi la Makorokocho

Akizungumza na EATV mmoja wa wanakundi hilo Hamadi Abasi amesema waliweka bayana msimamo wao kwamba kama wasiposhinda mwaka huu hawatashiriki tena na wakishinda pia hawatashiriki kwa kuwa mshindi hashiriki tena mwaka unaofuata.

“Sisi tuliweka wazi mapema msimamo wetu baada ya kuangalia wenzetu namna wanavyocheza tukagundua kuna gepu ambalo tukilifanyia kazi tutashinda, ndiyo maana kila siku sisi tumekuwa wabunifu kuanzia muonekano hadi mavazi na aina ya uchezaji” Amesema Hamadi.

Kwa upande wake Salum Abas amesema mchuano mwaka huu ulikuwa mkali sana jambo ambalo liliwafanya wao kudumu kwenye mazoezi kwa muda mrefu na kuhakikisha kila mmoja anakuwa tayari kwa mashindano.

Aidha kundi hilo limesifu uamuzi wa majaji kwamba haukuwa na upendeleo wa aina yoyote kwani kila mmoja uwanjani aliona uwezo wa kundi hilo na hivyo wanashukuru kwa majaji kutenda haki.

Fainali za Dance100% ambazo zimefanyika Jumamosi Septemba 24 Oysterbay Jijini Dar es Salaam zitaoneshwa na EATV siku ya Jumapili saa moja jioni.

Tags: