"Sipaki rangi za bei rahisi,kuanzia laki 1"- Rhino

Jumatatu , 12th Oct , 2020

Baada ya kuzungumziwa sana kwa kupaka rangi kucha zake msanii Rhino King amezua jipya kwa kujibu kuhusu hilo ambapo amesema hapaki rangi za bei rahisi,  gharama zake anazotumia yeye ni kuanzia shilingi laki 1.

Msanii Rhino King akiwa na rangi nyeusi kwenye kucha zake

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital Rhino King ameeleza kuwa "Nimeanza kupaka rangi kabla ya kuwa na Akida OG, lakini kaka yangu ndiyo amenibadilisha kutoka kwenye rangi za bei rahisi hadi za kwenye laki moja moja, zile za elfu 10 siwezi kupaka na nimeshaachana nazo"  

Licha ya Rhino King kusainiwa kwenye lebo mpya chini ya Mkurugenzi Akida OG, amesema bado yupo kwenye kundi la The Mafik japo wameshamaliza mkataba na aliyekuwa anawasimamia ambaye ni Director Msafiri.

Zaidi tazama hapa chini kwenye video.