Nandy ni noma, awamaliza Alikiba na Harmonize

Jumamosi , 14th Nov , 2020

Kwa haraka haraka unaweza kusema kwa mwaka huu 2020, Nandy 'The African Princess' ndiyo msanii wa kike aliyefanya vizuri zaidi kuliko wengine kwa sababu ya nyimbo zake kufanya ku-trend kwenye 'industry', chart za BongoFleva, mitandaoni na madili ambayo ameyapata.

Kushoto ni msanii Nandy akiwa na Alikiba, kulia akiwa na Harmonize

Nandy ameweza kutoa ngoma 5 ambazo ni na nusu, acha lizame ft Harmonize, dozi, 'do me' na Billnass, nyimbo zote hizo zimefanya vizuri kwenye chart za muziki wa BongoFleva na ya mwisho ni hii aliyotoa na Alikiba inaitwa nibakishie.

Na namba huwa hazidanganyi kwani video ya wimbo wake wa na nusu una watazamaji milioni 2 kwenye mtandao wa YouTube, video ya acha lizame ina watazamaji milioni 6.4, video ya dozi ina laki 7, na video ya 'do me' aliyofanya na Billnass ina watazamaji milioni 1.5.

Kubwa zaidi ni kufanya kazi kwa pamoja na wasanii wakubwa hapa nchini Tanzania ambao ni Harmonize kwenye wimbo wa acha lizame na hii mpya iitwayo nibakishie aliyomshirikisha Alikiba.

Kibiashara inaweza kuwa nzuri kwa upande wake kwani anaweza kuongeza mashabiki wapya kutoka kwa wasanii hao ambao wana nguvu kubwa ya mashabiki na mitandaoni au ngoma hizo kufanya vizuri kwa sababu ya kuwashirikisha kwenye ngoma zake.