Hamisa kumshtaki Kajala kisa Paula

Jumapili , 14th Feb , 2021

Baada ya kuhusishwa kwenye tukio la kusambaa video za mtoto wa Kajala, mwanamitindo Hamisa Mobetto amekanusha kuhusika.

Hamisa Mobetto na Paula

Ametoa ushahidi wa video kuwa siku ya Feb 9, 2021, ambayo imetajwa na Kajala kuwa ndio walitoka, Paula hakuwa na nywele zinazoonekana kwenye video.

Pia amesema atamshtaki Kajala kwa kumchafulia jina lake.

''Rest assured sitaliacha hili lipite bure, nafikiri itakuwa fundisho zuri na kwa wale wooooote ambao wamekua wakichafua jina langu kwa upuuzi wao'', ameandika Hamisa.