Country Boy asainiwa Konde Gang, apewa na gari juu

Ijumaa , 11th Sep , 2020

Baada ya kuwasaini wasanii Killy na Cheed mapema wiki hii, msanii na CEO wa Konde Gang Music, Harmonize ametangaza kusaini kichwa kingine cha muziki wa HipHop ambaye ni msaniii Country Boy.

Msanii Country Boy kushoto, kulia Harmonize

Harmonize amewatambulisha rasmi Country Boy, Cheed na Killy siku ya leo wakati anaongea na waandishi kuhusu show yake ya Father Night ambapo wasanii wake wote watakuwepo kwenye show hiyo atakayoifanya usiku wa leo kwenye makao makuu ya Konde Gang.  

Licha ya kuwatambulisha wasanii hao kwenye lebo ya Konde Gang, Harmonize amewafanyia Surprise wasanii wake ambao ni Country Boy na Ibraah Tz kwa kuwapa gari aina ya Crown kwa kila mmoja.

Kwa sasa Konde Gang ina jumla ya wasanii sita ambao ni Harmonize, Ibraah, Young Skales, Killy Cheed pamoja na Country Boy.