Jumamosi , 23rd Sep , 2017

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara timu ya Yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda FC kwenye mchezo uliomalizika jioni hii kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Bao pekee la ushindi kwa Yanga limefungwa na mshambuliaji wao Ibrahim Ajib dakika ya 34 kipindi cha kwanza.

Yanga sasa imefikisha alama 8 sawa na mahasimu wao Simba ambao wote wamecheza mechi 4. Simba anasalia katika nafasi ya pili kwa tofuati ya mabao ya kufunga na kufungwa huku Yanga ikiwa katika nafasi ya tatu wote wakisubiri matokeo ya klabu ya Azam FC kesho.

Katika michezo mingine iliyopigwa leo Majimaji wakiwa nyumbani wamekubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Njombe Mji. Mwadui nayo imekubali kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Tanzania Prisons.