Jumanne , 3rd Jun , 2014

Serikali ya Tanzania imesema imeweka mikakati mbalimbali ya kuwahudumia watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi ikiwa ni pamoja na kutoa huduma za tiba na matunzo pamoja na kuwaanzishia wagonjwa wapya dawa za kupunguza makali ya virus vya Ukimwi ARV.

Waziri wa afya na ustawi wa jamii nchini Tanzania Dkt Seif Rashid.

Akitoa hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa mwaka wa fedha 2014/2015, Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Seif Rashid amesema serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kwa kuanza kutoa dawa za kupunguza makali kwa mama na watoto waliobainika kuishi na virus hivyo.

Katika hatua nyingine, Dkt. Rashid amesema serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kukabiliana na magonjwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na maradhi ya malaria na ugonjwa wa dengue uliolipuka hivi karibuni.