Wezi wa magari watajwa

Monday , 17th Jul , 2017

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam limewakamata watu 250 kwa makosa mbalimbali ikiwamo usambazaji dawa za kulevya na wizi wa magari.

Kamanda Mkondya amewataja wanaotuhumiwa kuwa wezi wa magari ni Adam Hamisi (22) Adam Karubya na mwingine aliyetambuliwa kwa jina moja la Mangube (58) wakiwa na magari yanayodaiwa kuwa ni ya wizi.

Hayo yamebainishwa leo na Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Lucas Mkondya amesema jeshi hilo katika kipindi cha Julai 10 limefanikiwa kukamata watuhumiwa 250 kwa makosa mbalimbali ikiwamo usambazaji wa dawa za kulevya.

Amesema katika msako wake limefanikiwa kukamata bunduki moja aina ya shortgun na risasi tano, magari ya wizi na wauzaji wa gongo ambapo watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na watafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika.
 

Recent Posts

Winga wa Yanga SC, Simon Msuva

Sport
Msuva aiwaza La Liga

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Waziri Ummy Mwalimu

Current Affairs
Mganga Mfawidhi Mlandizi asimamishwa kazi