Jumatatu , 21st Dec , 2015

Waziri wa Afya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Ummy Mwalimu amemwagiza mganga mkuu wa hospitali ya rufaa Bombo,kuhakikisha madaktari wote wenye zamu kuwepo kwenye vituo vyao vya kazi muda wote wasisubiri waitwe

Waziri wa Afya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Ummy Mwalimu avamia hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga, kukagua utoaji wa huduma za afya jana

Mh. Ummy Mwalimu alimuagiza mganga mkuu huyo baada ya kufanya ziara katika hosptali ya Bombo Jijini Tanga ambapo alibaini kuwa madkatari wengi waliokuwepo zamu ni wanafunzi hivyo kuagiza lazima daktari wa zamu awepo kituoni kama ratiba yake ilivyopangwa.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy Mwalimu amewashauri wazazi nchini kuwapeleka watoto wadogo kwenye vituo vya afya badala ya kuwapatia dawa za mitishamba ili kupunguza athari na vifo vya watoto wachanga

Kaimu mganga mkuu wa mkoa wa tanga Dkt.Marcel clement ametoa ahadi kwa waziri huyo wa Afya na kusema kuwa changamoto alizozikuta watajitahidi kuzirekebisha ikiwemo usafi pamoja na madaktari kuwepo kazini kama ratiba yao inavyojieleza.