Jumapili , 15th Jun , 2014

Serikali ya Tanzania imekiri kuwa baadhi ya wamiliki wa vitalu katika ranchi za taifa mkoani Kagera wamekuwa wakikodisha ranchi hizo kwa watu wenye ng;ombe kutoka nchi za jirani badala ya kuzitumia kulisha mifugo yao.

Waziri wa maendeleo ya mifugo Dkt Titus Kamani.

Waziri wa maendeleo ya mifugo Dkt Titus Kamani amesema hayo wakati wa ziara ya kutembelea ranchi mbali mbali zilizopo mkoani Kagera, ziara ambayo imemkutanisha pia na wawekezaji wenye vitalu hivyo, wakulima pamoja na viongozi wa vijiji.

Kufuatia hali hiyo waziri Kamani amewaonya wanaofanya vitendo hivyo kuacha mara moja na kuahidi kuchukua hatua kali za kisheria kutokana na kile alichoeleza kuwa vitendo hivyo ni hujuma kwa uchumi wa nchi.