Ijumaa , 16th Mei , 2014

Wazazi nchini Tanzania wameaswa kuweka mazingira bora na ya usalama kwa watoto wao pale wanapowaacha majumbani na kwenda katika shughuli za ujenzi wa taifa ili kuwaepusha watoto hao na uwezekano wa kupata ugonjwa wa homa ya Dengue.

Mbu aina ya Aedes Egypti anayesambaza virusi vinavyosababisha homa hatari ya dengue.

Wito huo umetolewa leo Jijini Dar-es-Salaam na muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Agha Khan Love Luck mwasha wakati walipokuwa wakiendesha zoezi la usafi wa mazingira katika fukwe za bahari ya Hindi iliyopo karibu na hospitali hiyo.

Bi. Mwasha amesema iwapo wazazi watachukua tahadhari hiyo wataweza kupunguza madhara yanayotokana na ugonjwa wa Dengue kwa familia zinazobaki majumbani na kuongeza kwamba wananchi wa maeneo husika ndiyo wanapaswa kujitolea kufanya usafi wa mazingira na kuangamiza mazalia ya mbu.

Tags: