Jumanne , 15th Mar , 2016

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto, Ummy Mwalimu amesema bara la Afrika na hasa wanawake ndio wanaobeba mzigo zaidi wa madhara ya mabadiliko ya tabianchi,huku wakinyimwa fursa ya kushiriki kutafuta suluhu ya tatizo hilo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto, Ummy Mwalimu

Mhe. Ummy amesema hayo wakati akihutubia kikao cha 60 cha Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya wanawake, CSW60 kwa niaba ya kundi la nchi za Afrika,ambapo akisisitiza umuhimu wa kushirikisha zaidi wanawake katika uongozi wa kimataifa kuhusu suala la mabadiliko ya tabianchi.

Mhe. Ummy ameongeza kuwa wanawake wanapaswa kuongoza katika ngazi za kitaifa na serikali za mitaa na Ubunifu wao, ujuzi wa kiasili, matarajio yao yanaweza kusaidia katika kubuni na kushawishi suluhu kuhusu mabadiliko ya tabianchi.

Aidha amezungumzia suala la kilimo ambacho hushughulisha wanawake zaidi, akisema la msingi ni kusaidia sekta binafsi ili kukuza ukuaji wa uchumi katika sekta hiyo na hivyo kuwezesha wwanawake.