Alhamisi , 10th Sep , 2020

Wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi nchini Tanzania wameaswa kutumia lugha sahihi ya kiswahili inayoeleweka wakati wa uwasilishaji wa sera na ilani kwaajili ya kupewa ridhaa ya kuongoza katika nafasi hizo.

Wananchi wakisikiliza wagombea(hawapo pichani) wakinadi sera zao

Wito huo umetolewa na Mchunguzi wa Lugha mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) Ambrose Mghanga wakati wa mahojiani na EATV iliyotaka kufahamu mchango wao katika kusaidia watia nia wa nafasi mbalimbali katika uwasilishaji wa sera zao ambapo amesistiza kuwa zipo athari hasi endapo hawatumia lugha sahihi ya uwasilishaji ambayo inaweza kuzua machafuko au migongano baina ya wagombea wengine.

“Suala la lugha ni jabo muhimu sana mtu akishindwa kutumia lugha sanifu na staha italeta mdhara makubwa, sisi tunakemea hali hiyo kwani mtu anapotumia lugha nzuri inatoa nafasi kwa wananchi kuweza kuchambua na kuchagua viongozi sahihi”

Dkt Ahmed Sovu ni Mhadhiri wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere anaeleza kuhusiana na fursa za kilugha zainazoweza kupatikana kipindi hiki cha kampeni ikiwemo uandaaji wa hotuba kwa wagombea pamoja na kuzihariri hivyo kutoa wito kwa wamahiri wa lugha kujikita katika kusaidia wagombea ili waweze kuwasilisha sera zenye kueleweka kwa wananchi.

“Zipo fursa lufufu kwa sababu wagombea wanahitaji kuandaliwa hotuba, kuongeza matumizi ya misemo ambayo inarasimishwa kuwa misamiati ipo mingi kama hapa kazi, mabadiliko, mageuzi yote hii hutumiwa na wanasiasa zaidi kwa wasanii kuweza kuandaa nyimbo kwaajili ya motisha hivyo kuzalisha vipato na ajira zaidi” alisisitiza Dkt Sovu