Alhamisi , 22nd Mei , 2014

Serikali ya Tanzania imewataka waganga wa mikoa na wilaya nchini kuongeza juhudi katika kusimia usafi wa mazingira ili kutokomeza mazalia ya mbu anayeeneza uogonjwa wa Dengue.

Naibu waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii nchini Tanzania, Dkt Kebwe Stephen Kebwe.

Hayo yameelezwa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Kebwe Stephen Kebwe wakati akijibu maswali ya wabunge waliotaka kufahamu hatua za dharura zinazochukuliwa na serikali kudhibiti ugonjwa huo.

Kwa upande mwingine, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Samweli Sita wakati akitoa makadirio ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2014/2015 amesema serikali imepanga kupunguza vituo vya ukaguzi wa mizigo kutoka 15 hadi 3 ili kuimarisha usafirishaji wa bidhaa kati ya Tanzania na nchi za Rwanda na Burundi.