Alhamisi , 27th Aug , 2020

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominick, amewaondoa hofu wagombea waliowekewa pingamizi kwa kuwa pingamizi hizo ni kwa mujibu wa katiba na kuwataka watetetee pingamizi walizowekewa ndani ya muda uliopangwa kisheria.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominick akipokea fomu za mmoja wa wagombea Ubunge katika jimbo hilo

Mkurugenzi huyo amesema kuwa mpaka sasa Manispaa hiyo imeshapokea mapingamizi 11 kutoka vyama mbalimbali dhidi ya wagombea wa nafasi za Ubunge na Udiwani, hivyo kusisitiza waliowekewa mapingamizi kuwasilisha utetezi wao mapema.

Aidha ameongeza kuwa tayari wameshaanza mchakato wa kuyashughulikia mapingamizi hayo ili kila mgombea apate haki yake huku vyama vitano vikiwa vimeshapewa taarifa kuhusu mapingamizi hayo.

Mpaka sasa vyama mbalimbali vipo kwenye hatua ya kufanya kampeni kwenye maeneo mbalimbali nchini huku joto la uchanguzi likizidi kuchukua nafasi yake