Ijumaa , 10th Jul , 2015

Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Mh. Tundu Lissu amesema licha ya Tume ya Uchaguzi kuwa na mapungufu katika uandaaji wa mchakato wa uchaguzi mkuu watashiriki uchaguzi huo huku wakiwataka wananchi wajitokeze kwa wingi.

Mwanashria Mkuu wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo CHADEMA, Mh. Tundu Lissu

Mh. Lissu amesema kuwa licha ya Ubovu wa tume wanaoulalamikia kila siku kwa kuwa sio huri lakini kunakochangiua kuviangusha vyama vya upinzania ni baadhi ya wananchama wao kutofanya kwa Uadilifu.

Mh. Lissu ameongeza kuwa kati ya Mambo ambayo Chama cha kinasisitiza ni wananchi kujitokea kwa wingi katika kuiandikisha Katika Daftari la Kudumu la kupiga kura ili wananchi wapate haki yao ya kuwachagua viongozi wanaowataka.

Lissu amesema kuwa kama sheria na tume zinazotumika katika majimbo ambayo wamekishinda Chama Cha Mapinduzi kwanini wasiweze katika majimbo mengine na kusema yote hayo inatokana na uzembe wa baadhi ya wanachama wao kutofanya kazi vizuri.

Ameongeza kuwa siri ya ushindi kwa chama ni lazima kufanya kampeni ya kutosha kwa wananchi lakini pia kutafuta pesa kwa ajili ya kuweza kuzunguka kufanya kampeni pamoja na kuweka mawakala ambao wana uwezo mzuri wa kusimamia katika zoezi la kuhesabu kura.