Jumanne , 27th Sep , 2022

Wakati Mwenge wa uhuru ukimaliza kukagua na kutembelea miradi mbalimbali ndani ya Mkoa wa Katavi, umebaini dosari katika jengo la wagonjwa mahutututi katika hospitali ya wilaya ya Tanganyika, ambapo moja ya chumba kimebainika kufungwa taa za mwanga kama wa disko (dicso light).

Taa za disko

Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Sahili Geraruma, ameshangwazwa na wataalamu waliosimamia ujenzi wa majengo hayo kwa kutokuwa ya kisasa.

Akiendelea kubainisha dosari kiongozi huyo hajapendezwa pia na namna ambavyo mabomba yalivyotapakaa ukutani na kusema ujenzi huo sio wa kisasa.