Jumanne , 8th Mar , 2016

Leo ikiwa ni siku ya Wanawake Dunia,Serikali ya Tanzania imesema kuwa itaongeza nguvu katika mikakati ya kufikia asilimia hamsini kwa hamsini ya ushirika wa wanawake na wanaume katika fursa mbalimbali za kisiasa,kiuchumi na kijamii.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu.

Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu, wakati wa mkutano wa maandalizi ya sherehe ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka March 8.

Waziri Mwalimu amesema kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha inawawezesha wanawake kisheria, Kiuchumi, kuongeza ushiriki katika ngazi ya maamuzi na fursa sawa katika Elimu,Mafunzo na Ajira.

Aidha Mhe. Mwalimu amesisitiza kuibua mipango na kuonyesha muitikio wa utekelezaji wa maazimio yaliyopo hususani yanayolenga kuimrisha usawa wa kijinsia katika nyanja zote.

Waziri Mwalimu ameongeza kwa kusema kuwa changamoto nyingine kubwa ambayo ameahidi kuifanyika kazi kwa kupeleka bungeni mswaada wa sheria wa marekebisho ya sheria ya ndoa za utotoni ambazo zimekua ni kikwazo kwa watoto wengi wa kike kupiga hatua kimaendeleo.

Ummy Mwalimu amesema kuwa hata uwiano wa Wanafunzi wa kike na wa kiume katika Elimu ya Juu ni tofauti hivyo watafanya kila jitihada kuweza kuweka uwiano wa asilimia hamsini kwa hamsini.