Ijumaa , 15th Jul , 2016

Serikali ya Tanzania imesema imewapeleka madaktari wa magonjwa mbalimbali nchini India kwa ajili ya kupata mafunzo na uzoefu ili kupunguza wimbi la wagonjwa wanaokwenda kutibiwa nje kwa gharama za serikali.

Katibu Mkuu wa Wizara ya ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya

Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam,Katibu Mkuu wa Wizara ya ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema hatua pia itasaidia kusaidia sekta ya Afya kwa kiasi kikubwa.

Aidha Dkt. Ulisubisya amesema tayari serikali imeziagiza taasisi mbalimbali za kiserikali zinatoa huduma za kiafya kuboresha mazingira ya watumishi wao ikiwemo kutoa motisha kwa wafanyakazi hao kupitia mapato ya ndani ya taasisi zao ili koboresha zaidi huduma za kiafya kupita watumishi hao.

Amesema kuwa upungufu wa madaktari hao ambao wameenda kupata uzoefu ni pamoja madaktari katika idara ya Koo,Pua, Masikio, Figo, na Tumbo ambapo watakaporejewa kutakua hakuna ulzima wa kuwasafirisha wagonjwa wenye matatizo hayo kwenda nje ya nchi.

Katibu Mkuu amesema pia Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ipo katika mpango wa kuboresha mejngo yake ikiwa ni pamoja na kuongeza vyumba vya uapsuaji kwa watoto ili kuondoa mlolongo mrefu wa watoto hao kufanyiwa upasuaji.

Ameongeza kuwa pia huduma ya magonjwa ya nje kwa tafiti walizofanya imeboreka kwa kuwa madaktari kwa wanapatikana muda wote kutoa huduma kwa wagonjwa.

Sauti ya Katibu Mkuu wa Wizara ya ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya.