Jumatatu , 18th Apr , 2016

Serikali imeamua kuyafungua machinjio ya Vingunguti Jijini Dar es Salaam kwa muda wakati matengenezo yakiendelea ili kutatua tatizo la ukosefu wa nyama ulioanza kujitokeza jijini baada ya machinjio hayo kufungwa kwa muda.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba wakijadiliana.

Wakiongea katika machijio hayo mara baada ya kufanya ziara katika Machinjio hayo Waziri wa Kilimo na Mifugo Mhe. Mwigulu Nchemba, na Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu wamesema licha ya kufungua machijio hayo lazima marekebisho mengine yaendelee.

Mhe. Mwiguli amewataka wachinjaji wajipange katika siku tatu waweze kuchinja huku wakiendelea na ukarabati wa machinjio hayo huku Mhe. Ummy akitoa maelekezo ya kuwa na mazingira safi ya machinjio hayo.

Kwa upande wao wafanyabiashra wa nyama wamesema wamekua wakipata tabu kwenda kuchinjia mbali wakati maeneo yote ya machinjio hali zake ni sawa, huku wakiitaka serikali kuongeza eneo hilo la machinjio ambapo hapo awali walikua wanachinja Ng'ombe 50 lakini kwa sasa wanachinja zaidi ya ng'ombe 500.

Sauti ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba wakielezea ufunguaji wa Machinjio hayo.