Jumanne , 28th Jun , 2016

Serikali imesema kuwa ina mkakati mahsusi wa kuhakikisha wanaongeza kiasi cha madaktari ambao wamesajiliwa kwa ajili ya kutoa huduma za afya ili kuwa na madkatari wengi zaidi wanaofanyakazi kwenye serikali.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Hamis Kigwangalla.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Hamis Kigwangalla, akiongea jana bungeni mjini Dodoma amesema kuwa licha ya kuwa na wahitimu wengi wa masomo ya udaktari lakini bado kumekuwepo na tatizo la upugufu wa madaktari.

Mhe. Kigwangalla amesema kuwa serikali imezidi kuboresha maslahi ya madaktari wa serikali ili waendelee kufanya kazi kwa weledi na mpaka sasa wamefanikisha hilo kwa kuwa kwa sasa madaktari wengi wa serikali wanalipwa vizuri zaidi kuliko waliopo kwenye sekta binafsi.

Aidha, amesema kuwa serikali haiwezi kuwabana madaktari wanaokwenda kufanya kazi nje ya nchi kwa kuwa ni fursa ya kujiongezea kipato na ujuzi zaidi na kusema ili kudhibiti hilo serikali itaboresha zaidi maslahi ya madaktari ili wengi waweze kuendelea kufanya kazi nchini.