Ijumaa , 3rd Jul , 2015

Uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura BVR, ulioahirishwa kwa mikoa ya Dar es salaam na Pwani, utaanza Julai 16 hadi 25 kwa Dar es Salaam na Julai 7 hadi 20 kwa Pwani.

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, Julius Mallaba.

Taarifa hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, Julius Mallaba kwa vyombo vya habari na kuwataka wananchi wote wa mikoa hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye vituo vya uandikishaji.

Uandikishwaji wa daftari hilo uliahirishwa kutokana na kuchelewa kwa vifaa kutoka mikoani kwa ajili ya kuongezea ufanisi kutokana na maeneo hayo kuwa na idadi kubwa ya watu wenye sifa ya kuandikishwa.

Aidha Mallaba amewataka wale wote wenye kadi za kupigia kura za zamani waende nazo ili kurahisisha uchukuaji wa taarifa zao na kadi hizo zitarudishwa NEC.