Mwigulu ajibu kuhusu mienendo ya benki

Jumatano , 3rd Feb , 2021

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Mwigulu Nchemba  amesema Banki Kuu ya Tanzania (BoT) inafuatilia mienendo ya mabenki nchini ili kuokoa fedha za wananchi ambao wanahifadhi akiba ya fedha zao katika mabenki hayo.

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Mwigulu Nchemba

Dkt. Mwigulu ametoa kauli hiyo Bungeni leo Jijini Dodoma baada ya baadhi ya wabunge kutaka kujua hatima na haki za wateja ambao benki zao zinafungwa kutokana na matatizo mbalimbali.

Katika kipindi hicho cha maswali na majibu bungeni baadhi ya wabunge walitaka kujua hatma ya mashamba ambayo hayaendelezwi nakubakia kugeuka vichaka ambavyo mazingira yake si rafiki kwa wananchi wanaokaa katika maeneo jirani na mapori hayo.

Mkutano wa pili kikao cha pili cha Bunge la 12 umeendelea kwa wabunge kuchangia hotuba ya Rais. Dk. John Pombe Magufuli aliyoitoa wakati akifungua bunge.

Tazama video hapo chini