Mgombea Ubunge aliyefariki dunia kuzikwa leo

Jumanne , 15th Sep , 2020

Aliyekuwa mgombea Ubunge wa jimbo la Mpendae kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Salim Turky, ambaye amefariki usiku wa kuamkia leo Sep 15, 2020, atazikwa leo Saa 10:00 Jioni huko Fuoni Kijito Upele mkoa wa Mjini Magharibi.

Salim Turky

Salim Turky alikua ni Mbunge wa Jimbo la Mpendae miaka mitano iliyopita na pia alikua mgombea ubunge katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28, ambapo imeelezwa kuwa na hata juzi katika ufunguzi wa kampeni za CCM Zanzibar uliofanyika viwanja vya Demokrasia Mjini Unguja.

Katika uzinduzi huo Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein, alimpa fursa ya kujinadi na kuomba kura kwa wanachama wa CCM wa Jimbo la Mpendae ambao waliohudhuria. 

Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwake Mpendae na maiti itaswaliwa katika Masjid  Muhammad (Msikiti wa Othman Maalim), uliopo Mchina Mwanzo na marehemu atazikwa Fuoni Kijito Upele Mkoa wa Mjini Magharibi.