Jumatatu , 14th Sep , 2015

Mauzo katika soko la hisa la Dar es Salaam—DSE yameshuka kwa asilimia 62 kutoka shilingi bilioni 6.4 hadi shilingi bilioni 2.4 kwa mujibu wa takwimu za biashara na mauzo katika soko hilo katika kipindi cha juma moja lililopita.

Meneja Miradi na Biashara wa Soko la Hisa (DSE) Bw. Patrick Mususa.

Meneja Miradi wa DSE Bw. Patrick Mususa, amesema hayo jijini Dar es Salaam leo na kusema kuwa mtaji katika soko bado unaonyesha mwelekeo chanya ambapo katika kipindi hicho mtaji umeongezeka kutoka shilingi trilioni 21.9 hadi shilingi trilioni ushirini na mbili nukta tatu.

Kwa upande wa viashiria vya soko, Mususa amesema amesema kiashiria cha sekta ya huduma za kibenki na kifedha kimeshuka huku kiashiria cha sekta ya viwanda kikiwa kimeongezeka kiasi.

Kwa ujumla, Mususa amesema idadi ya mauzo katika soko hilo imekuwa kijiendesha katika hali yake ya kawaida katika kipindi cha majuma mawili yaliyopita.