Jumatatu , 13th Apr , 2015

Mauzo katika Soko la Hisa la Dar es salaam yameshuka kwa asilimia 1.5 toka Bilion 8.6 hadi bilion 7.6 huku wastan wa hisa zilizouzwa kwa wiki iliyopita ikipungua pia kwa asilimia 88.63

Meneja Fedha na Utafiti wa DSE Mshindo Ibrahimu.

Akizungumza na Hotmix Meneja Fedha na Utafiti wa DSE Mshindo Ibrahimu amesema kuwa sababu kubwa ya kushuka kwa mauzo hayo ni sikukuu mfululizo toka Ijumaa kuu mpaka kumbukumbu ya Abeid Aman Karume.

Kwa Upande wa Sekta zilizochangia Mauzo makubwa sokoni hapo ni Sekta ya viwanda kwa asilimia 97 ikifuatiwa na Sekta ya Fedha kwa asilimia 1.2 huku wawekezaji toka nje wakiongoza kwa kuwekeza kuliko wawekezaji wa ndani.

Hata hivyo pamoja na kushuka kwa mauzo sokoni hapo biashara imepanda kwa asilimia 1 ambayo ni kubwa kibiashara..