Jumapili , 2nd Aug , 2015

Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Feruzy Bano ametangaza matokeo ya kura za maoni Jimbo la Aru

Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Feruzy Bano ametangaza matokeo ya kura za maoni Jimbo la Arusha Mjini mapema leo, nakusema kwa sasa hawezi kusema aliyeshinda kw akura ndio mshindi, sababu bado wana vikao vya kuchunja na atakayerudishwa jina lake ndio atakayepeperusha bendera.

Amewataja wagombea na kura zao kuwa ni Philemon Monaban (5320) akifuatiwa na Justin Nyari (1894), Moses Mwizarubi (1005), Reuben Mwiteni (171), Thomas Munisi (832),Victor Njau (752), Emmanuel Ole Njoro (90),Mohammed Omary (171), Swalehe Kiluvia (446), Hamisi Migire (305), Weraufoo Munisi (832) na Mustafa Panju (498).

Baada ya kumaliza kuwatangaza wagombea hao na kura zao, alizuia watu kushngilia sana kwa madai kuwa kuna vikao vya uteuzi vinaendelea.

Hata hivyo wakati wakitangaza matokeo hayo wagombea waliokuwepo watatu ambao ni Philemon Monaban, Justin Nyari na Mustafa Panju na wengine wote hawakuwepo kwa madai kuwa wamechakachuliwa kura zao na hawajaridhika na matokeo.