Jumapili , 6th Feb , 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema serikali itaendelea kutoa fedha kwaajili ya kuanzisha miradi mipya na kukamilisha iliyoanza.

Rais Samia (kushoto) na moja ya miradi (kulia)

Rais Samia amesema hayo leo Jumapili Februari 6, 2022 wakati akiweka jiwe la Msingi kwenye ujenzi wa mradi wa maji Mungango, Kiabakari mkoani Mara.

“Najua ndugu zangu, kulikuwa na vineno neno kadhaa, elimu haitaendelea, miradi haitaendelea na mambo mengine kadhaa lakini nadhani mnajionea wenyewe kwa macho yenu kwamba miradi inaendelea na inaendelezwa kuliko ilivyokuwa ikiendela,” amesema Rais Samia Suluhu Hassan.

Aidha ameongeza kuwa, “Tutakwenda kutafuta sababu ya kwanini kuna kusuasua kwa miradi ndani ya mkoa huu, na pengine tuitafutie dawa, kwahiyo mkiona tunachukua vijihatua, mjue tunatafuta dawa ya kuacha miradi kusuasua”.