Ijumaa , 17th Sep , 2021

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jafo amepiga marufuku uingizwaji wa bidhaa zinazozalisha hewa isiyo salama kwa binadamu hasa kwa bidhaa zinazotumia gesi Zikiwemo za majokofu na viyoyozi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jafo

Mhe. Jafo ameyabainisha hayo Jijini Dodoma kwenye ukaguzi wa maeneo ya mafundi mchundo na maeneo ambayo yanazalisha vifaa vinavyotumia gesi ambapo ameagiza wafanyabiashara na wawekezaji kuacha kujihusisha na bidhaa hizo na badala yake waweke bidhaa rafiki kwa mazingira ili kuondokana na uharibifu wa tabaka la hewa na kuendana na mabadiliko ya tabia nchi.

Tazama video hapo chini