Jumanne , 4th Aug , 2015

Mgombea wa Nafasi ya Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, Dkt. John Magufuli leo anatarajia kuchukua fomu ya kugombea kiti hicho katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC jijini Dar es Salaam.

Mh. John Pombe magufuli akiwa na Mgombea Mwenza Samia Suluhu wakati wakitambulishwa

Ratiba hiyo ilitolewa jana Jijini Dar es Salaam na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipozungumza na Waandishi wa Habari na kusema zoezi hilo litafanyika leo saa tano asubuhi akisindikizwa na viongozi na wanachama wa chama hicho.

Wakati huo huo amesema vikao vya juu vya vya chama hicho vinatarajia kuanza keshokutwa kwa ajili ya kujadili na kupitisha majina ya wagombea wa nafasi za Ubunge na Udiwani.

Dkt. Magufuli alishashinda uteuzi wa kuwa Mgombea Urais wa CCM katika vikao vyake vilivyofanyika mjini Dodoma mapema mwezi uliopita akiwashinda wenzake 38 ambao walikua miongoni mwa 42 waliochukua fomu