Alhamisi , 2nd Jul , 2015

Spika wa Bunge Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda amelazimika kusitisha kikao cha Bunge leo asubuhi baada ya baadhi ya wabunge kusimama kupinga utaratibu wa uwasilishwaji miswada.

Spika wa Bunge Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Anne Makinda.

Hatua hiyo ilifikiwa baada ya mbunge wa Ubungo John Mnyika kuomba muongozo wa utaratibu uliotumika juu ya uwasilishwaji wa miswada mitatu kwa hati ya Dharura kinyume na makubaliano yaliyofikiwa na wabunge kuhusu uwasilishwaji wake wa miswada hiyo.

Mnyika amesema kuwa wabunge kwa kauli moja walikubaliana na walikataa kwamba miswada hiyo isiwasilishwe kwa hati ya dharura na isije kwa utaratibu wa kuwasilishwa kwa pamoja.

Miswada hiyo ambayo imekataliwa kuwasilishwa leo ni pamoja na muswada wa sheria ya Petroli wa mwaka 2015, muswada wa sheria ya usimamizi wa mapato ya mafuta na gesi ya mwaka 2015 na muswada wa sheria ya uwazi na uwajibikaji katika tasnia ya uchimbaji Tanzania ya mwaka 2015.

Akitoa muongozo Spika Makinda alisema kuwa hakuna sheria iliyokiukwa katika uwaslishwaji wa miswada hiyo na kusema makubaliano yao ndiyo yaliyofanya kuwasilishwa kwa miswada hiyo hali iliyopelekea baadhi ya wabunge kusimama na kupinga kauli hiyo ya Spika.

Sikiliza hapa hali ilivyokuwa............